Raia wa Marekani Terry Ray Kreiger kusalia seli siku 9 kwenye kesi ya kudhulumu watoto kingono

  • | Citizen TV
    3,137 views

    Terry Ray Kreiger, raia wa Marekani anayedaiwa kuwadhulumu kingono watoto watatu katika mtaa wa Great Wall Gardens, Athi River atasalia korokoroni kwa siku tisa zaidi baada ya kukana mashtaka kumi na moja dhidi yake. Kwenye kesi mbili alizosomewa leo, Ray alikabiliwa na mashtaka sita ikiwemo dhuluma dhidi ya watoto, kuwepo nchini kinyume cha sheria na kujihusisha na biashara ya ngono ya watoto. Raia huyo wa marekani alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 50 mwaka wa 2014 baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza picha zake akishiriki ngono na watoto.