Raila adai Rais Ruto anataka kuteka idara ya mahakama

  • | Citizen TV
    1,819 views

    Kinara wa Azimio La Umoja Raila Odinga ameendelea kumshtumu Rais William Ruto kwa madai ya njama ya kuteka nyara mahakama. Akikosoa mkutano wa rais na jaji mkuu martha koome katika ikulu ya Nairobi, Raila amesisitiza kuwa mkutano huo ulikuwa na njama fiche ya kutangaza nafasi za ajira katika mahakama kuu ili kumpa rais ruto nafasi ya kuchagua watu wake.