Raila akutana na Senata Chris Coons wa Marekani

  • | Citizen TV
    3,929 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga leo amefanya mkutano na seneta wa jimbo la Delaware nchini Marekani Chris Coons huku vikao vya kamati ya mazungumzo ya uwiano vikitarajiwa kurejelewa hapo kesho. Japo ajenda ya mazungumzo ya Odinga na Coons yakiwa yamefichwa, Odinga kupitia mtandao wa Twitter alikiri kuwa na kikao naye huku duru zikiarifu kuwa yaliyojadiliwa ni pamoja na mazungumzo yanayoenedelea kule Bomas baina ya waakilishi serikali na upinzani.