Raila alaani hatua ya Rais ya kuwaachisha kazi kwa muda makamishna wanne wa tume ya uchaguzi IEBC

  • | K24 Video
    395 views

    Kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga amelaani hatua ya rais William Ruto kuwaachisha kazi kwa muda makamishna wanne wa tume ya uchaguzi IEBC pamoja na kubuni jopo la kuwachunguza litakaloongozwa na jaji wa mahakama ya rufaa Aggrey Muchelule . Odinga sasa anasema demokrasia ya taifa iko mashakani, na kuwa ataandaa maandamano na mikutano ya umma kuanzia tarehe saba mwezi huu na kutoa thabiti sikukuu ya jamhuri. Siku hiyo ataongoza taifa kwa maombi katika uwanja wa kamukunji. hatahivyo mmoja wa makamishna hao, justus nyagaya amejiuzulu.