Raila amsuta Rais Ruto kwa kutema ndoto za waanzilishi wa taifa

  • | K24 Video
    123 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga amemsuta rais William Ruto kwa kutema ndoto za waanzilishi wa taifa waliokusudia wakenya wawe na maisha bora. Odinga aliyekuwa katika kaunti ya Kwale kuendelza juhudi za kuzolea chama chake cha ODM umaarufu amesema kuwa Ruto amewageuka wakenya na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi kwani sasa hawawezi kujimudu kiafya, kielimu na hata kuwa na bidhaa za msingi. Chama cha ODM pia kinalalamika kuhusu kile wanachodai ni hatua ya serikali ya kulemaza vyama vya kisiasa kwa kuvinyima fedha.