Raila asema treni ya BBI imeanza safari na haiwezi kusimamishwa

  • | KBC Video
    Naibu wa Rais Dkt. William Ruto amesema hakuna dharura ya kufanya marekebisho ya katiba.Ruto ambaye alikuwa akiongea katika eneo bunge la Narok magharibi katika kaunti ya Narok alisema hatakubali kushinikizwa kujihusisha na shughuli ambayo huenda ikaigawanya nchi hii.Alisema hayo huku kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akiendelea na ziara yake katika eneo la pwani ambapo alipokuwa Malindi alidai kwamba treni ya BBI imeanza safari na haiwezi kusimamishwa hasa baada ya BBI kuungwa mkono na mabunge mengi ya kaunti. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive