Raila ataka serikali iwalipe fidia waathiriwa wa mkasa wa mlipuko wa gesi shilingi nusu milioni

  • | K24 Video
    33 views

    Kinara wa Azimio Raila Odinga ametaka serikali iwalipe fidia waathiriwa wa mkasa wa mlipuko wa gesi ya isiyopungua shilingi nusu milioni kila mmoja. Odinga aliyezidi kuisuta serikali kwa kuzembea, ametaka wakuu wa mamlaka ya EPRA wafutwe kazi mara moja kwa kile alichokitaja kama kukithiri kwa ufisadi ambao ulichangia kuwekwa kwa viwanda vya gesi katika maeneo ya makaazi. Mkasa huo uliua watu 6 huku zaidi ya watu mia tatu wakijeruhiwa.