Raila, Karua waongoza kwa umaarufu wa urais jijini Nairobi

  • | Citizen TV
    733 views

    Asilimia 49 ya wakazi wa Nairobi wangempigia kura mgombea wa urais wa Azimio Raila Odinga iwapo uchaguzi ungefanyika leo. Hii ni kulingana na utafiti wa kampuni ya Infotrak . Kulingana na utafiti huo naibu rais ambaye ni mgombea wa Kenya Kwanza William Ruto angepigiwa kura na asilimia 30 ya wakaazi wa Nairobi, huku asilimia tano wakimuunga mkono mgombea wa Roots party George Wajakoyah. Katika kinyanganyiro cha ugavana Johnson Sakaja anaongoza kwa asilimia 39, Polycarp Igathe akiwa wa pili na asilimia 33 na kufuatwa na Agnes Kagure aliye na asilimia 0.4. Edwin Sifuna ana umaarufu katika kinyanganyiro cha Seneta jijini akiongoza kwa asilimia 44 na kufuatwa kwa karibu na Margaret Wanjiru aliye na asilimia 12. Kando na umaarufu wa kisiasa asilimia 73 ya wakazi wa Nairobi wanahisi kuwa taifa haliendi katika njia sawa. Utafiti uliofanywa tarehe 2 na tatu mwezi huu uliwahusisha wakazi 1,024 wa kaunti ya Nairobi .