Raila Odinga aapa kupinga sera za Rais William Ruto kupitia mikutano ya hadhara kote nchini

  • | KTN News
    3,137 views

    Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ameapa kupinga sera za Rais William Ruto kupitia mikutano ya hadhara kote nchini. Akizungumza mjini kisumu siku ya jumapili Odinga amesema gharama ya juu ya maisha na kukosa kutekelezwa kwa baadhi ya ahadi za serikali ni baadhi ya sababu za kufanya uamuzi huo. Waziri huyo mkuu wa zamani aidha amesema siku ya jumatano wataandaa mkutano maarufu kama kamukunji jijini Nairobi utakaowaleta pamoja viongozi kutoka Nyanza, Pwani, Nairobi na maeneo mengine.