Raila Odinga asema maandamano ya kuskuma serikali ishushe gharama ya Maisha itaanza wiki ijayo

  • | Citizen TV
    3,762 views

    Muungano wa upinzani umetangaza kuendeleza maandamano wiki ijayo wakati makataa ya siku 14 ulioipa serikali kupunguza gharama ya maisha yatakapokamilika. kwenye hafla ya mazishi ya Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa jamii ya Waluo Ker Willis Opiyo Otondi huko Nyahera kaunti ya Kisumu, Viongozi wa upinzani wamesema serikali ya William Ruto imepuuza matakwa yao ya kupunguzwa kwa gharama ya maisha. Viongozi hao wakiongozwa na kinara wa azimio Raila Odinga wameshutumu serikali kwa kufeli kutimiza ahadi ya kushusha gharama ya maisha.