Rais aagiza mashauriano ya nyongeza ya 6% ya kiwango cha chini cha mishahara ya wafanyikazi

  • | KBC Video
    19 views

    Rais William Ruto amemwagiza waziri wa leba Florence Bore kuongoza mchakato wa kuongeza kiwango cha chini cha mishahara ya wafanyikazi kwa angalau asilimia sita kutokana na mchango wao muhimu katika ujenzi wa taifa. Rais aliyasema haya wakati sherehe za 59 za siku kuu ya leba katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi alipokuwa akijibu ombi la katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyikazi-COTU Francis Atwoli ambaye alikuwa akiomba nyongeza ya asilimia 22.5 ya kiwango cha chini cha mishahara ya wafanyikazi ili kuwakinga kutokana na hali ngumu za kiuchumi. Giverson Maina anatuarifu zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive