Rais ametaka wazazi wajihusishe na elimu ya wana wao

  • | K24 Video
    75 views

    Rais William Ruto amewashawishi wazazi wasiwaachie walimu majukumu yote ya malezi. Haya yanajiri baada ya ripoti ya jopo la kutathmini sekta ya elimu kuonyesha kuwa wazazi wengi wangependa kutohusishwa katika ufanikishaji wa mtaala wa CBC. Akiunga mkono mapendekezo yaliyowasilishwa kwake, rais Ruto amesema mabadiliko kidogo yatatekelezwa ili kuboresha mtaala huo, pia amefahamisha kuwa rasilimali zitawasilishwa kwa wakati ufaao ili kukamilisha ujenzi wa madarasa na maabara katika shule za msingi. Ripoti hiyo imeendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa wazazi na wadau wa elimu kote nchini.