Rais Biden awaasa Warepublikan kuepusha mzozo mwengine wa kupelekea serikali kufungwa

  • | VOA Swahili
    549 views
    Mswaada wa kufadhili Bunge la Marekani uliopitishwa Jumamosi na kusainiwa na Rais Joe Biden uliepusha serikali kufungwa na utaiwezesha serikali kuendelea na kazi zake hadi katikati ya mwezi Novemba. Hata hivyo Rais alionya kuhusu hali hiyo kujirudia tena. Ungana na mwandishi wetu akukuletea hoja ya Rais Biden kuhusu kuepuka kutokea mzozo mwengine. Endelea kusikiliza... #mswaada #ufadhili #bunge #marekani #rais #joebiden #serikali #mzozo #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.