Rais Museveni anaomba muhula mwingine wa urais

  • | BBC Swahili
    1,918 views
    Rais Yoweri Kaguta Museveni anaomba muhula mwingine wa urais – kwa mara ya saba! Akiwa na umri wa miaka 80, Museveni amechukua fomu ya kugombea tena urais kupitia chama chake cha National Resistance Movement (NRM) ambayo inatokana na vuguvugu la National Resistance Army iliyomleta madarakani mwaka 1986 kama kiongozi wa waasi. Akihutubia wafuasi wake jijini Kampala, alisema: “Safari hii, lazima tupambane na rushwa kwa nguvu zote.” Lakini wakosoaji wake wanasema si rushwa tu — bali ni kutotaka kuachia madaraka. Bosha Nyanje anatuelezea taarifa hii: #bbcswahili #Madaraka #Uganda #uchaguzi #siasa #utawala #museveni Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw