- 204 viewsDuration: 1:12Rais William Ruto ameagiza idara ya Jeshi la Kenya kusimamia ujenzi wa uwanja wa Kidundu katika kaunti ya Vihiga, zoezi ambalo limelengwa kukamilika katika muda wa miezi 9 ijayo. Uwanja huo una bajeti ya shilingi milioni 900 na utakuwa mojawapo ya miradi muhimu katika kaunti ya Vihiga.