Rais Ruto aahidi Harambee Stars zawadi nono kwa ushindi katika mechi za CHAN

  • | Citizen TV
    766 views

    Rais william ruto ameahidi kuwatunukia zawadi nono wachezaji wa timu ya taifa ya Harambee Stars watakaoshiriki kwenye kivumbi cha chan kwa mara ya kwanza. Rais Ruto ameahidi timu hiyo zawadi ya shilingi milioni mia sita iwapo itatwaa kombe la chan 2024. Kwa kila mechi ambapo harambee stars itavuna ushindi, rais ameahidi shilingi milioni moja kwa kila mchezaji. Na kama anavyoarifu willy lusige, rais aliwapa motisha wachezaji alipowatembelea kambini mapema leo.