Rais Ruto aahidi uchunguzi kamili wa ajali iliyomuua Jenerali Ogolla

  • | Citizen TV
    6,494 views

    Rais William Ruto ameahidi kuwa uchunguzi wa ajali ya ndege iliyomuua mkuu wa majeshi Jenerali Francis Ogolla itawekwa bayana pindi tu itakapokamilika. Rais Ruto akisema kuwa anatarajia uchunguzi wa kina kuhusiana na ajali hiyo ambayo pia iliwaangamiza wanajeshi wengine tisa. Rais amesema hayo baada ya viongozi wa upinzani kutaka uchunguzi huo kukamilishwa haraka na wananchi kufahamishwa yaliyosababisha kuanguka kwa ndege iliyowabeba maafisa hao huko Elgeyo Marakwet. Nimrod Taabu amekuwa Siaya na kutuandalia taarifa ifuatayo