Rais Ruto aapa kuwaunga mkono wanariadha wa Kenya wanaojiandaa kushiriki katika michezo ya Olimpiki

  • | K24 Video
    83 views

    Rais William Ruto ameapa kuwaunga mkono wanariadha wa Kenya wanaojiandaa kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao jijini Paris, Ufaransa. Wanariadha Faith Kipyegon na Mary Moraa waliotia fora katika mashindano ya ubingwa wa dunia wa riadha yaliyokuwa jijini Budapest Hungary, walipewa ahadi hiyo hii leo na rais William Ruto, katika ikulu ya Nairobi. Mabingwa hao jana walituzwa jumla ya shilingi milioni kwa kushinda nishani za dhahabu.