Rais Ruto akashifu wanaopinga kukodiwa viwanda

  • | Citizen TV
    2,319 views

    Rais William Ruto sasa amewakashifu viongozi wanaopinga ukodeshwaji wa viwanda vinne vya sukari, na kusema kuwa sharti viwanda hivyo viendeshwe na wawekezaji wa kibinafsi. Akizungumza katika Ikulu, Ruto alisema kuwa taifa linapania kupiga buti suala la uagizaji kwa kufufua viwanda vya humu nchini. Haya yanajiri huku ripoti za hivi punde zikibahsiri kupungua kwa usagaji wa sukari kutokana na uhaba wa miwa.