Rais Ruto akutana na viongozi wa nyanza kujadili miradi ya maendeleo

  • | Citizen TV
    935 views

    Rais William Ruto alikutana na wabunge kutoka eneo la Nyanza katika ikulu ya Nairobi na kuwaahidi kuwa hatabagua eneo lolote nchini kimaendeleo. Rais Ruto amesema atafanya kazi na viongozi wote bila kujali mrengo wa kisiasa wanaoegemea ili kuhakikisha maendeleo sawa nchini. Rais amesema ni haki ya kila Mkenya kupata huduma za serikali iwe walimpigia kura au la.