Rais Ruto ampa mwaka mmoja Waziri Murkomen kuwajibika

  • | Citizen TV
    1,804 views

    Rais William Ruto sasa amempa waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen mwaka mmoja kuhakikisha kuwa ajali za barabarani nchini zinapungua. Akizungumza katika uzinduzi wa kanuni mpya za usalama wa barabarani hii leo, Rais Ruto alisema kuwa ni jukumu la wizara ya uchukuzi kukaza kamba katika utekelezwaji wa kanuni za usalama ili kupunguza maafa barabarani. Haya yanajiri huku takwimu za hivi punde zikiashiria kuwa zaidi ya watu elfu moja wamepoteza maisha katika muda wa miezi minne iliyopita. Kanuni zilizozinduliwa hii leo zinashirikisha matumizi ya teknolojia barabarani