Rais Ruto amteua Mohamed Amin kuwa bosi mpya wa Idara ya DCI

  • | K24 Video
    31 views

    Mohamed Amin Ibrahim ndiye mkurugenzi mpya wa idara ya upelelezi wa jinai,DCI. Amin ambaye alikuwa mkurugenzi wa kitengo cha masuala ya ndani katika huduma ya polisi, sasa anachukua nafasi ya George Kinoti, ambaye alijiuzulu hivi majuzi mwanzoni mwa uongozi mpya wa rais William Ruto. Rais Ruto alimteua amin miongoni mwa watatu waliopendekezwa kwake.