Skip to main content
Skip to main content

Rais Ruto anaendelea na ziara ya maendeleo Laikipia

  • | Citizen TV
    164 views
    Rais William Ruto hii leo anazuru kaunti ya Laikipia ambapo amezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha huduma centre katika eneo la doldol huko Laikipia kaskazini. Kituo hicho kitawawezesha wakazi hawa kupata huduma za serikali karibu nao. Aidha Rais ameahidi kuwa ujenzi wa Barabara kuu ya kilomita 60 kutoka Nanyuki kuelekea doldol utaanza katika muda wa wiki mbili zijazo akiongeza kwamba kaunti hii itanufaika na kilomita 217 zaidi za lami kutoka kwa serikali yake. Rais pia alishutumu viongozi wa upinzani akisema kwamba lengo lao ni kuwapotosha wananchi kwani hawana la kuwafanyia isipokuwa kupiga siasa.