Rais Ruto aongoza mkutano wa mawaziri wa serikali iliyopita ikulu ya Nairobi

  • | Citizen TV
    14,461 views

    Rais William Ruto ameongoza mkutano wa baraza la mawaziri katika ikulu ya Rais hii leo, huu ukiwa mkutano wa pili tangu alipotwaa rasmi uongozi. Mkutano huu unaohudhuriwa na mawaziri wanaoondoka wa serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta unatarajiwa kuangazia sera na baadhi ya maswala ambayo Rais anataka yashughulikiwe kabla ya baraza lake la mawaziri kupigwa msasa na bunge na kuidhinishwa kuanza kazi rasmi. Kati ya maswala haya huenda ni maswala yanayohusiana na sekta ya pamba aliyowaahidi wakaazi wa Homa Bay alipozuru hapo jana. Aidha rais aliahidi nyumba za bei nafuu kwa wakazi