Rais Ruto aonya dhidi ya uharibu wa mali katika maandamano ya Azimio

  • | K24 Video
    132 views

    Rais William Ruto ameonya dhidi ya uharibu wa mali katika maandamano ya muungano wa Azimio yanayonuiwa kufanyika hapo kesho. Akihutubia sherehe za siku ya wafanyakazi katika bustani ya uhuru, rais amesema, ingawaje katiba inaruhusu maandamano, katiba hio pia imeipa jukumu serikali kutumia mbinu zozote kulinda maisha na mali ya watu. Hata hivyo, naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito kwa upinzani na kinara wake Raila Odinga kuzingatia mazungumzo badala ya maandamano. Maoni hayo yamepigiwa upato na katibu mkuu wa muugano wa wafanyikazi COTU Francis Atwoli.