Rais Ruto apongeza idara ya misitu nchini

  • | Citizen TV
    439 views

    Rais William Ruto amepongeza usimamizi wa shirika la misitu nchini kwa kuongeza mapato ya shirika hilo katika kipindi cha chini ya miaka miwili . Rais Ruto ambaye amezungumza katika hafla ya kufuzu kwa maafisa wa misitu eneo la Gilgil kaunti ya Nakuru ,amesifia mashirika ya kiserikali ambayo anasema yameongeza mapato yao, jambo ambalo limesaidia kupunguza matumizi ya fedha zilizotengwa na serikali. Ruto aidha amewarai wakenya kuwa na imani na nchi yao na kuwataka wasiskize uvumi. Mahafala mia tano sabini na wanne wamefuzu hii leo ambapo ni idadi kubwa zaidi ya waliofuzu tangu kenya ilipopata uhuru.