Rais Ruto asema mpango wa afya kwa wote utaanza Januari mwakani

  • | Citizen TV
    1,655 views

    Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itaanza kutekeleza mpango wa Afya kwa Wote kuanzia januari mosi mwakani, akisema kuwa vikao vya umma kuhusu kanuni za mpango huu vitaanza wiki ijayo. Rais William Ruto sasa akiagiza shirika la usambazaji dawa na huduma za matibabu KEMSA na lile la MEDS , kushirikiana katika kununua na kusambaza vifaa vya matibabu kote nchini kwa lengo la kupunguza gharama za huduma za afya. Rais alizungumza kaunti ya Machakos wakati wa kuzinduliwa rasmi kwa maabara ya kisasa. Maabara hiyo ni ya pili ya aina yake nchini na inatarajiwa kuimarisha utafiti wa kimaabara nchini