- 2,402 viewsRais William Ruto amesema kamwe hatakubali mageuzi ya katiba kumpa muda zaidi wa kuhudumu kama Rais. Rais badala yake akisema wale wanaoeneza fikra za kuongeza muda wake wa kuhudumu hawafahamu uzito wa majukumu ya kuwa rais. Matamshi ya rais yakijiri baada ya misururu ya matamshi ya baadhi ya wanasiasa na wandani wake kuhusu haja ya kumuongeza muda wa kuhudumu.