Rais Ruto ataka sheria kuhakikisha mgombea mwenza ni mwanamke

  • | Citizen TV
    1,364 views

    Rais William Ruto ameahidi kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa usawa wa thuluthi mbili wa uwakilishi wa kijinsia umeafikiwa katika nafasi za uongozi chini ya serikali yake. Ruto, aliyehutubia mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa kundi la wanawake magavana la G7 hapa Nairobi, amemtaka mwenyekiti wa chama cha UDA Cecily Mbarire kubuni sheria zitakazofanikisha mgombea urais wa kiume kuwa na mgombea mwenza wa kike. Ahadi inayoonekana kuwa huenda ikabadilisha baadhi ya maagano ya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2027.