Rais Ruto ataka wafadhili kuchangia dola 120 kwa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

  • | Citizen TV
    1,247 views

    Viongozi wa bara Afrika wanayataka mataifa yaliyostawi kufadhili riba ya chini ya mikopo inayotolewa na benki ya dunia kwa mataifa yanayostawi ili kuyawezesha kufanikisha miradi ya maendeleo na kukabili mabadiliko ya tabianchi. Rais William Ruto, ambaye anaongoza mkutano wa viongozi wa mataifa 20 ya bara afrika humu nchini amesema mataifa yaliyostawi yanafaa kutoa mchango wa angalau dola bilioni 120 kufanikisha mipango ya maendeleo afrika. aidha rais amesema bara afrika linalemewa na mzigo wa madeni unaotishia kulemaza uchumi, na kadhalika majanga ya njaa na mafuriko. Ruto ameyataka mataifa yaliyostawi kuchukua hatua za dharura ili kuinusuru Afrika. Wafadhili watatangaza michango yao mwezi Disemba kwenye kongamano litakalofanyika nchini Japan.