- 14,503 viewsDuration: 2:56Rais William Ruto amelaumu utepetevu wa baadhi ya mataifa akiyalaumu kwa kile anasema ni kurudisha nyuma harakati za kuleta amani nchiini Haiti. Rais akisema kuwa licha ya ahadi nyingi zilizotolewa, ni mataifa machache pekee yaliyojitolea kwa hali na mali katika juhudi hizo. Akizungumza jijini New York nchini Marekani, Rais pia ameshikilia kuwa Kenya haitaondoka Haiti hadi wakati taifa hilo litaweza kujisimamia.