- 1,253 viewsDuration: 3:41Tukirejelea utata unaokumba Nairobi Hospital ni kuwa, Rais William Ruto amesema kuwa aliamuru kukamatwa na kuondolewa mamlakani kwa maafisa wanne wanaohusishwa na usimamizi wa hospitali hiyo kwa madai ya ufisadi na utumizi mbaya wa mamlaka. Akizungumza huko Mlima Elgon wakati wa ziara yake eneo la magharibi, Rais Ruto alisisitiza kwamba kamwe hatakubali wale anaodai kuwa 'mafisadi' kuongoza hospitali hiyo ambayo inatambulika kwa kutoa huduma za hali ya juu za matibabu.