- 4,392 viewsDuration: 3:17Rais William Ruto ametangaza kuundwa kwa kamati maalum ya watu wanane ya kutekeleza ushirikiano kati ya chama cha ODM na UDA, na kusaidia kutekelezwa kwa ripoti ya ajenda kumi za ushirikiano wa vyama hivi viwili. Akizungumza alipopokea ripoti hiyo hapa Nairobi, rais Ruto pamoja na kinara wa ODM Dkt. Oburu Oginga waliwashambulia wanaopinga ripoti hiyo, wakisema itasaidia kuwaunganisha wakenya