Rais Ruto awaomba wakenya wawe na subra na kumruhusu atekeleze mikakati aliyonayo

  • | K24 Video
    105 views

    Rais William Ruto amewaomba wakenya wawe na subra na kumruhusu atekeleze mikakati aliyonayo kuboresha uchumi wa taifa. Akitetea mapendekezo ya mswada wa fedha wa 2023, Ruto amesema kuwa ushuru unaolengwa kukusanywa na serikali si kwa manufaa ya watu binafsi, bali huo ndio utakaotumika kutimiza ahadi walizotoa kwa wakenya. Vilevile amedokeza kuwa hali ya uchumi ikiimarika huenda ushuru ukapunguzwa