Rais Ruto awatahadharisha viongozi wanaokwepa kulipa ushuru

  • | KBC Video
    24 views

    Rais William Ruto amesifia mikakati iliyowekwa na halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini KRA ya kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji ushuru na udhibiti wa viwango nchini. Akiongea huko Mombasa wakati wa maadhimisho ya siku ya ulipaji ushuru, kiongozi wa taifa alisema serikali itachukulia hatua kali dhidi ya mashirika na watu binafsi wanaokosa kulipa ushuru. Rais alikariri kuwa serikali haitavumilia ufisadi huku akiwaagiza maafisa wote wakuu wa serikali na jamii kuzingatia sheria zilizowekwa. Juney karisa anasimulia zaidi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News