Rais Ruto awataka mawaziri na makatibu wake kuwajibika katika utendakazi wao

  • | Citizen TV
    11,754 views

    Rais Ruto amewakaripia mawaziri na makatibu wake akiwataka kuwajibika katika utendakazi wao. Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini mikataba ya utendakazi itakayotumika kuchunguza shughuli za maafisa wakuu serikalini, rais alielezea kutamaushwa kwake na baadhi ya mawaziri na makatibu ambao walionekana kutoelewa majukumu yao.