Rais Ruto azidi kukosoa maandamano yanayofanywa na upinzani

  • | Citizen TV
    3,398 views

    Rais William Ruto ameendelea kukashifu maandamano ya upinzani akilaumu azimio kwa kusababisha hasara kubwa nchini. Akizungumza kaunti ya Taita Taveta, Rais Ruto kwa mara nyingine tena ametetea polisi kufuatia shutuma za kutumia nguvu kupita kiasi kutawanya waandamanaji akisema hataruhusu polisi kuvamiwa ilhali wana jukumu la kulinda maisha na mali ya Wakenya.