Skip to main content
Skip to main content

Rais Ruto hatinaye atoa taarifa kuhusu mvutano na utata wa Nairobi Hospital

  • | Citizen TV
    8,236 views
    Duration: 4:03
    Rais William Ruto amethibitisha kuingilia mvutano wa uongozi katika Nairobi Hospital. Kwenye Taarifa yake, Rais alithibitisha kukutana na wale aliowataja kuwa wadau wa hospitali hiyo ambao walitafuta usaidizi wake kutatua mgogoro wa bodi ya usimamizi wa hospitali hiyo ya kibinafsi. Rais pia alikiri kuwa aliwapa majukumu mkuu wa utumishi wa Umma Felix Kosgei na mwanasheria mkuu Dorcas Oduor kuongoza kundi la mashirika kadhaa ya serikali kuchunguza shughuli za hospitali hiyo. Usiku wa Jumatatu Runinga ya Citizen ilitoa taarifa ya kipekee kuhusu jinsi serikali ilivyohusika katika mgogoro wa bodi ya usimamizi wa hospitali hiyo. Rais Ruto amethibitisha kuhusika kwake akisema usaidizi wake ulitafutwa kutokana na majukumu yake kama mlezi wa chama cha hospitali nchini kinachomiliki hospitali hiyo.