Rais Ruto pia apigia upato kuwa na Naibu Rais wa kike

  • | Citizen TV
    945 views

    Rais William Ruto ameahidi kuwa ataendelea kujitolea kuhakikisha kuwa usawa wa thuluthi mbili za kijinsia umeafikiwa chini ya serikali yake ya Kenya Kwanza. Rais aidha amesema kuwa serikali yake imeendelea kuchukua hatua kufanikisha hili. Alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa kundi la wanawake magavana la G7 hapa Nairobi, ambapo amemtaka mwenyekiti wa UDA Cecily Mbarire kubuni sheria zitakazofanikisha mgombea urais wa kiume kuwa na mgombea mwenza wa kike