Rais wa shirikisho la kandanda nchini, FKF Hussein Mohammed amesema huenda malumbano yanayoshuhudiwa katika shirikisho hilo yakasambaratisha nafasi ya Kenya kuwa mwenyeji wa kipute cha AFCON 2027.. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge ya michezo, Mohamed amesisitiza kuwa yeye bado ndiye Rais wa shirikisho hilo na atasalia ofisini kuendelea na majukumu yake. Kumekuwa na mvutano kuhusu uongozi wa FKF, pande mbili zikizozana kufuatia madai ya ubadhirifu wa fedha. Hivi sasa naibu Rais wa shirikisho hilo Mac Donald Mariga yuko mbele ya kamati hiyo, Mariga akiongoza upade wa pili wa mzozo huo.