Rais wa Marekani alaani mapinduzi Afrika, ahimiza demokrasia

  • | VOA Swahili
    2,342 views
    Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne alihutubia kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, akigusia masuala kadhaa, kati ya hayo ni umuhimu wa kuheshimu maadili ya kidemokrasia na pia mapinduzi ya kijeshi Afrika. Wakati akitoa hotuba yake Biden alisema Washington “iliitisha Mkutano wa Demokrasia kuziimarisha taasisi za kidemokrasia, kupambana na ufisadi na kupinga ghasia za kisiasa,” akiongeza , “na wakati huu, ambapo serikali zilizo chaguliwa kidemokrasia zimepinduliwa zikifuatana kwa haraka huko Afrika Magharibi na Kati, inatukumbusha kuwa kazi hii ni muhimu na ya haraka kama ilivyokuwa siku zote. #unga #voaunga #unga78 #biden #AU #AfricanUnion #ECOWAS