Rais wa Russia azuru UAE na Saudi Arabia, aongoza ujumbe mzito kutoka Kremlin

  • | VOA Swahili
    2,743 views
    Rais wa Russia Vladimir Putin amezuru Umoja wa Falme za Kiarabu Jumatano. Pia amefanya ziara huko Saudi Arabia ambako amekutana na Prince Mohammed bin Salman. Alipowasili Abu Dhabi Rais Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan alimlaki “rafiki ” yake na ndege za kivita za UAE zilitoa salamu kwa mkuu wa Kremlin kwa kupita huku zikiacha nyuma alama ya rangi mbalimbali za bendera ya Russia. Ujumbe wa Russia ulikuwa na maafisa mbalimbali wa ngazi ya juu kutoka sekta ya mafuta, uchumi, mambo ya nje, anga za juu na nishati ya nyuklia. Haikufahamika mara moja nini Putin, ambaye ni nadra kwake kuondoka Russia tangu kuanza kwa vita vya Ukraine, anataka hasa kujadili kuhusu mafuta au siasa za kieneo atapokutana na Prince Mohammed bin Salman nchi inayo safirisha mafuta ghafi kwa wingi zaidi duniani. - Reuters #russia #kremlin #vladimirputin #rais #sheikh #mohammedbinZayed #alnahyan #saudiarabia #abudhabi #prince #mohammedbinsalman