Rais William Ruto ajitokeza na kuwahakikishia wakenya kwamba serikali yake iko imara kuiongoza taifa

  • | KTN News
    5,620 views

    Rais William Ruto amejitokeza na kuwahakikishia wakenya kwamba serikali yake iko imara katika kuliongoza taifa akisema kelele zinazoshuhudiwa nchini ni ishara tosha kuwa kila mmoja anatekeleza majukumu yake. Ruto ambaye alikuwa akizungumza wakati wa ibada ya jumapili eneo la Karen amesema atatekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa wakenya. Kwa upande wake Naibu Rais Rigathi Gachagua ametetea ziara za Ruto nje ya nchi.