Rais William Ruto atia sahihi mswada wa fedha mwaka 2023 na sasa umekuwa sheria

  • | Citizen TV
    1,188 views

    Rais William Ruto ametia mswada wa fedha mwaka 2023 na sasa umekuwa sheria. Mswada huo ulipitishwa na bunge la kitaifa wiki jana baada ya vikao kadhaa vikiwemo maoni kutoka kwa wananchi. Kulikuwa na pingamizi kuhusu baadhi ya mapendekezo yaliyokuwa kwenye mswada huo likiwemo lile la ushuru wa asilimia 1.5 wa nyumba pamoja na kuongeza ushuru wa bidhaa za petroli kutoka asilimia 8 hadi 16. Sheria hiyo sasa itaanza kutekelezwa.