Rais William Ruto aunga mkono kufungwa kwa vilabu

  • | Citizen TV
    6,586 views

    Rais William Ruto ameunga mkono juhudi za gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kupiga marufuku vilabu vya usiku kwenye maeneo ya makaazi kufuatia malalamishi ya umma. Rais Ruto aliahidi kusimama na gavana Sakaja kuhakikisha kuwa viwango vya makaazi yasiyo kelele Nairobi vinaafikiwa. Rais alikuwa akizungumza alipozindua kituo cha usambazaji chakula cha kampuni ya Twiga ambapo ameahidi kushirikiana na kampuni hii kuwafikia wakulima na wafanyibiashara wadogo zaidi