Rais William Ruto awakashifu majenerali hasimu wa Sudan

  • | Citizen TV
    1,351 views

    Mgogoro wa kidiplomasia unaendelea kutokota baina ya Kenya na Sudan huku Kenya ikidaiwa kuhusika kwenye mzozo unaoendelea sudan, baada ya viongozi wa rsf kukutana nairobi mwezi februari mwaka huu na kutangaza serikali mpya sambamba na iliyopo. Rais William Ruto ametoa tahadhari kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Sudan, akionya kuwa vita hivyo vinaelekea kuwa mauaji ya halaiki huku majenerali wawili hasimu wakikosa kuonyesha nia ya kutamatisha vita hivyo. Rais Ruto ameyataka mataifa mengine kuingilia kati upesi kusitisha mgogoro huo. Ruto alitoa kauli hiyo katika ikulu ya nairobi alipokutana na rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar.