Rais William Ruto awaonya vijana wa Gen Z

  • | Citizen TV
    34,271 views

    Maandamano ya ukumbusho wa Vijana wa Gen Z yalipokuwa yakiendelea maeneo mbalimbali nchini, Rais William Ruto, ambaye alikuwa mjini Kilifi katika hafla ya Mazishi amewashauri vijana waliokuwa wakiandamana kutii sheria ata wakati wanapojieleza barabarani. Hafla hiyo pia ikihudhuriwa na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ambaye alikariri msimamo wake kwamba waathiriwa wa maandamano wanapaswa kufidiwa.