- 20,264 viewsDuration: 3:18Waziri wa zamani Raphael Tuju alifurushwa kwa nguvu na maafisa wa polisi usiku wa kuamkia Jumamosi kutoka katika eneo la biashara la Dari mtaani Karen, Nairobi. Tukio hilo linahusishwa na mzozo wa kisheria kuhusu mnada wa mali yake kutokana na deni la mkopo wa shilingi bilioni 2.2 analodaiwa na benki ya EADB. Hata hivyo, Tuju anasisitiza kuwa kufurushwa kwake hakukufuata sheria.