RBA yaonya wanaokosa kuwasilisha makato ya kustaafu

  • | Citizen TV
    220 views

    Mamlaka ya malipo ya kustaafu -RBA- imesema itatumia njia zote za kisheria kuhakikisha taasisi za serikali ambazo hazijatuma pensheni ya wafanyikazi wao kwenye akaunti husika zimefanya hivyo kwa haraka. Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Charles Machira amesema hatua hii inalenga kampuni za kibinafsi ambazo haziwazilishi pesa za wafanyikazi wao kwa mpango ya pensheni. Akizungumza mjini Garissa wakati wa kutoa uhamasisho kwa umma kuhusu umuhimu wa kujiunga na mipango ya pensheni, Machira alisema ni 26% ya wafanyikazi pekee wamejisajili kupokea pensheni yaani kati ya watu kumi, watu saba wako kwenye hatari ya ufukara baada ya kustaafu.