Rebecca Miano huenda akawa mwanasheria mkuu wa kwanza wa kike nchini

  • | Citizen TV
    2,482 views

    Rebecca Miano huenda akawa mwanasheria mkuu wa kwanza wa kike nchini, endapo bunge litamuidhinisha kwa wadhifa huo. Uteuzi wake kama mwanasheria pia ukifungua ukurasa wa kuzidi kupiga jeki uongozi wa kike kwenye fani za kisheria. Endapo ataidhinishwa na bunge kwa wadhifa huu, Miano atajiunga na Martha Koome na kikosi chake katika idara ya mahakama na hata nguvu kazi mpya ya Faith Odhiambo anayeongoza chama cha wanasheria nchini LSK.